Timu yarejea mazoezini kujiandaa na Wydad

Kikosi chetu kimefanya mazoezi katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca utakaopigwa Jumanne saa 10 jioni katika Uwanja wa Azam Complex.

Baada ya ushindi wa jana dhidi ya Kagera Sugar leo kikosi kimeendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo huo ambao tunahitaji alama tatu kwa kila hali.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na wapo kwenye hali na morali zikiwa juu hasa zikichagizwa na ushindi tuliopata jana.

Katika mchezo dhidi ya Wydad tutawakosa nyota wetu wawili Sadio Kanoute na Said Ntibazonkiza kwakuwa wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER