Timu yarejea Dar

Kikosi chetu kimerejea leo jijini Dar es Salaam kikitokea mkoani Mtwara baada ya mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup uliopigwa jana Uwanja wa Nangwanda Sijaona dhidi ya Azam FC tukapoteza kwa mabao 2-1.

Kikosi kimewasili mchana na wachezaji wamepewa ruhusu ya kwenda kupumzika.

Kesho jioni kikosi kitarejea tena mazoezini katika Uwanja wa Mo Simba Arena kuanza maandalizi ya mchezo unaofuata wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ruvu Shooting.

Mchezo dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa siku ya Ijumaaa May 12, saa 1:00 Usiku katika Uwanja wa Azam Complex.

Kwa sasa tumebakisha michezo mitatu ya ligi kuu ukiwemo wa Ijumaa na miwili ya mwisho itakuwa dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. Msimu unaokuja tunaomba viongozi waongeze umakini katika usajili!! Ni afadhali kusajili WACHEZAJI watatu tu wenye quality kuliko kuleta kundi la WACHEZAJI!! Harafu kocha aaminiwe apewe muda kila msimu tunakuwa na makocha zaidi ya watatu!!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER