Timu yaingia kambini kujiandaa na Azam

Baada ya mazoezi ya jana kikosi kimeingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC utakaopigwa kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna yoyote ambaye amepata maumivu yatakayomfanya kukosa mchezo wa kesho.

Baada ya mchezo wa juzi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca juzi, jana tumeanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Azam moja kwa moja na lengo ni kuhakikisha tunashinda.

Viingilio vya mchezo ni kama ifuatavyo:

Mzungo Sh. 5000
VIP B na C na Sh. 10,000
VIP A Sh. 15,000

Kama kawaida mchezo wetu wa kesho utapigwa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER