Timu yafanya mazoezi jioni kujiandaa na KMC

Kikosi chetu kimefanya mazoezi jioni katika Uwanja wa Shirika la Reli (TRC) mkoani hapa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC utakaopigwa Ijumaa katika Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi.

Timu iliwasili saa tano asubuhi ambapo wachezaji walipumzika kwa saa nne kabla ya kuanza mazoezi ya kuweka miili sawa.

Wachezaji wote 24 waliosafiri wamefanya mazoezi na wapo kwenye hali nzuri hakuna aliyepata majeraha.

Aidha, kikosi kinatarajia kufanya mazoezi ya mwisho kesho kabla ya kushuka dimbani.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER