Timu yafanya mazoezi asubuhi kuivutia kasi Coastal

Kikosi chetu kimefanya mazoezi katika uwanja wetu wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Alhamisi katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga.

Kikosi kimeingia kambini baada ya mazoezi ya jana jioni na kuanza maandalizi moja kwa moja kutokana na kumaliza majukumu ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo tumetinga robo fainali.

Wachezaji wote wako katika hali nzuri na tumerejesha nguvu zote kwenye ligi na kila mchezo tunauchukulia kama fainali pointi tatu ndiyo kipaumbele chetu.

Baada ya kumaliza mazoezi kikosi cha wachezaji 25 kitasafiri mchana kuelekea jijini Tanga tayari kwa mchezo dhidi ya Coastal Union.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER