Timu yaendelea na mazoezi Mo Arena

Timu yetu imeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers utakaopigwa Jumanne.

Kikosi kimeingia kambini baada ya mazoezi ya jana jioni ya kujiandaa na mchezo huo ambao hatuitajitaji chochote zaidi ya ushindi.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi isipokuwa Kibu Denis ambaye amefanya peke yake chini ya uangalizi wa daktari kutokana na kupata maumivu katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa nchini Uganda.

Morali za wachezaji ipo juu na wanafanya jitihada kubwa mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kuwapa nafasi katika mchezo wa Jumanne.

Mchezo wetu dhidi ya Vipers itapigwa saa moja usiku katika dimba la Benjamin Mkapa na tayari vituo vimetangazwa ambapo tiketi zinapatikana.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER