Kikosi chetu kitaondoka nchini Alhamisi kuelekea Misri tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi (Pre Season) 2022/23.
Wachezaji wote ambao tutakuwa nao msimu ujao watakuwepo safarini isipokuwa wale ambao watakuwa kwenye majukumu ya timu za taifa ambao watajiunga haraka wakimaliza.
Kambi hiyo ya mwezi mmoja itakuwa katika Mji wa Ismailia ambao tunaamini utamsaidia Kocha Zoran Maki na wasaidizi wake kukiandaa kikosi.
Kikosi kitarejea nchini Agosti 5 na Agosti 13 tutashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Yanga kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya NBC.