Timu kuondoka usiku kuifuata Mbeya City

Kikosi chetu kitaondoka leo saa tano usiku kuelekea jijini Mbeya tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Jumatano saa 10 jioni Uwanja wa Sokoine.

Kikosi kitaondoka na wachezaji 22 kuelekea jijini Mbeya kikiwa kamili kwa mpambano huo ambao tunaamini utakuwa mgumu kutokana na upinzani tunaokutana nao hasa wakiwa nyumbani.

Baada ya kufika timu itafanya mazoezi ya mwisho kesho saa 10 jioni katika Uwanja wa Sokoine kujiweka tayari kwa mtanange wa Jumatano.

Wachezaji wote ambao wapo kwenye orodha ya safari hali yao ni nzuri tayari kuipigania timu ugenini kutafuta alama tatu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER