Kikosi chetu kinatarajia kuondoka nchini kesho saa 10 alfajiri kuelekea Guinea tayari kwa mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya utakaopigiwa Jumamosi saa moja usiku.
Kikosi kitaondoka na msafara wa watu 45 ambapo wachezaji watakuwa 25 benchi la ufundi pamoja na viongozi.
Timu itasafiri na ndege ya Shirika la Ndege ya Ethiopia (Ethiopia Airlines) kikosi kitapitia nchini Ethiopia na kubadili ndege mpaka Guinea ambapo tunategemea kufika kesho jioni.
Tunatarajia kikosi kitakapofika nchini Guinea wachezaji kitafanya mazoezi ya utimamu wa mwili kuondoa uchovu wa safari.