Timu kuingia kambini kesho

Kikosi chetu kitaingia kambini kesho mchana kuanza maandalizi ya mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gandarmerie utakaopigwa Aprili 3, Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Wachezaji waliokuwa wameitwa kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) nao watajumuika kikosini baada ya kuombewa ruhusa na uongozi kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kujiondoa kambi ya Stars ambayo inajiandaa na mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Sudan.

Peter Banda ambaye pia aliitwa Timu ya Taifa ya Malawi naye ameombewa ruhusa ya kutokwenda kujiunga na atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaoingia kambini.

Hadi sasa hakuna mchezaji majeruhi hivyo wote waliosajiliwa kwa ajili ya mashindano ya CAF wataingia kambini kesho tayari kwa maandalizi ya mchezo huo.

Mchezo dhidi ya USGN tumeupa umuhimu mkubwa na tunauchukulia kama fainali kwa sababu ni ushindi tu ndiyo utatupa nafasi ya kutinga robo fainali.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER