Kikosi chetu jioni ya leo kitaingia kambini kujiandaa na mchezo wa hatua ya tatu ya Michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa Jumanne Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Wachezaji wote wataingia kambini huku wale ambao wanaendelea kupona majeraha yao nao wakiwepo.
Baada ya mchezo wa jana dhidi ya Yanga wachezaji waliruhusiwa kurudi nyumbani kuonana na familia zao na jioni wakimaliza mazoezi wanaingia kambini moja kwa moja.
Kutetea ubingwa wa michuano hii ni moja ya malengo yetu msimu huu wa Ligi 2021/22.
One Response