Simba yazidi kujifua nchini Morocco
Kikosi chetu leo Ijumaa Agosti 20 kimetimiza siku 10 nchini Morocco ambapo kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi 2021/22.
Wachezaji wote wapya tuliowasajili wapo hapa wakiendelea kuzoeana na wenzao wakiwa tayari kwa ajili ya msimu mpya.
Wachezaji wote wana ari ya kutaka kuonyesha uwezo ili kulishawishi benchi la ufundi hali inayoonyesha ushindani wa namba utakuwa mkubwa msimu huu.
Tunatarajia kucheza mechi moja ya kirafiki wikiendi hii lakini bado hatujajua itakuwa dhidi ya timu gani kwani mchakato bado unaendelea ili kuweka vitu sawa.
Baada ya mchezo wa wikiendi kikosi kitaendelea na maandalizi hapa Morocco wakati wachezaji walioitwa timu za taifa wakiruhusiwa kurejea kwenda kujiandaa na kufuzu fainali za kombe la dunia.