Simba yarejea Mwanza kuisubiri Kagera Sugar

Kikosi chetu leo kimerejea jijini Mwanza ambapo moja kwa moja kimeanza maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Jumatano katika Uwanja wa Kaitaba.

Baada ya kuwasili jijini hapa kikosi kimefanya mazoezi leo jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kuweka miili sawa kutokana na kazi kubwa waliyofanya jana katika mchezo dhidi ya Mwadui.

Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na hakuna yoyote aliyepata majeraha wala adhabu ya kadi hivyo kila mmoja yupo kamili kwa mechi ya Jumatano.

Timu ilifika Mwanza Aprili 16 juzi ikaelekea Shinyanga ilipocheza na Mwadui jana kabla ya kurejea tena leo kuendelea na maandalizi.

Baada ya mchezo dhidi ya Kagera timu itarudi tena jijini hapa kujiandaa na mchezo dhidi ya Gwambina FC ambao utakamilisha ziara yetu ya mechi za Kanda ya Ziwa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER