Kikosi chetu cha Simba Queens kimetinga fainali ya Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Yanga Princess kwa mikwaju ya penati 5-4 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Mchezo huo ambao tulitawala sehemu kubwa ulimalizika kwa sare ya bila kufungana huku wachezaji wetu wakipoteza nafasi nyingi za wazi.
Kama wachezaji wetu wangeongeza umakini katika nafasi tulizotengeneza tulikuwa tuna uwezo wa kuimaliza mechi ndani ya dakika 90.
Kocha Mkuu, Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa joanitha Ainembabazi na Elizabeth Mutukiza na kuwaingiza Aisha Juma na Esther Mayala.
Penati zetu zote tano zilifungwa na Esther Mayala, Aisha Juma, Mwanahamis Omary, Ruth Ingosi na Vivian Corazone.
Queens itakutana na JKT Queens iliyoifunga Fountain Gate kwa mabao 5-0 katika mchezo wa fainali utakaopigwa Disemba 12 katika Uwanja wa Azam Complex.