Simba Queens ya 2021/22 ni moto, yashusha majembe kama yote

Kikosi chetu cha Timu ya Wanawake cha Simba Queens kimeendelea kusukwa vikali kuelekea msimu mpya wa ligi 2021/22 ambao unaanza Alhamisi wiki hii.

Tayari tumeshusha nyota watatu kutoka mataifa makubwa barani Afrika kuungana na wenzao tayari kuanza msimu mpya.

Tayari kiungo mshambuliaji nyota Barakat Kikelomo Olaiya kutoka Bayhesa Queens ya Nigeria ameshatua kwa ajili ya kuongeza ubunifu kikosini.

Mbali na Barakati pia tumesajili mshambuliaji, Sabinah Thom raia wa Malawi kutoka D.D. Sunshine ambaye pia anaweza kucheza winga zote.

Mwingine ambaye tayari tumemtambulisha ni mshambuliaji, Pambani Falonne Kuzoya kutoka FCF Amani ya DR Congo.

Usajili huu mkubwa umefanywa kwa lengo moja tu kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu ili iwe mara ya tatu mfululizo na kuweka historia.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER