Simba kuwaonyesha Ruvu Shooting kilichomnyoa Namungo, Dilunga kulianzisha

Kiungo mshambuliaji Hassan Dilunga, lea ataanza kwenye kikosi cha kwanza kilichopangwa kuikabili Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba leo saa 10 jioni.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Namungo FC uliopigwa Jumamosi iliyopita Dilunga aliingia kutokea benchi na kuonyesha kiwango safi na kutoa pasi mpenyezo kwa Shomari Kapombe aliyepiga krosi ambayo ilimkuta Chris Mugalu na kutufungia bao la kusawazisha kwenye ushindi wa mabao 3-1.

Dilunga amepangwa kiungo ushambuliaji akitokea kulia huku Kocha Didier Gomes akiwaanzisha washambuliaji wawili John Bocco na Chris Mugalu ili kuhakikisha mabao yanapatikana mapema.

Erasto Nyoni ameanza katika eneo la ulinzi wa kati pamoja na Kennedy Juma akichukua nafasi ya Pascal Wawa aliyepumzishwa kutokana na kucheza mechi nyingi.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Taddeo Lwanga (4), Hassan Dilunga (24), Rally Bwalya (8), John Bocco (22), Chris Mugalu (7), Luis Miquissone (11).

Wachezaji wa Akiba – Beno Kakolanya (30), Said Ndemla (13), Bernard Morrison (3), Mzamiru Yassin (19), Medie Kagere (14), Miraji Athumani (21) David Kameta (27).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER