Sakho aitwa timu ya Taifa ya Senegal

Kiungo mshambuliaji, Pape Sakho amejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 24 cha timu ya taifa ya Senegal ‘Simba wa Terenga’ kitachocheza mechi mbili za kufuzu michuano ya AFCON dhidi ya Msumbiji.

Sakho ambaye ni mfungaji wa goli bora la Afrika mwaka jana anakuwa mchezaji pekee kutoka Afrika kuitwa kwenye kikosi cha Aliou Cisse.

Baada ya kumaliza mchezo wetu wa kesho wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya, Sakho atapata ruhusa ya kwenda kujiunga na Simba wa Terenga.

Nyota wengine wa kimataifa walioitwa timu zao Taifa ni:

Henock Inonga, DR Congo

Clatous Chama, Zambia

Peter Banda, Malawi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER