Robertinho: Tunaendelea kuwapa nafasi nyota wapya

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema nyota wapya tuliowasajili msimu huu wanazidi kupewa nafasi na wanaonyesha uwezo mkubwa ambapo wanaingia taratibu kikosini.

Robertinho amesema wachezaji tuliowasajili wanaonyesha kiwango bora na kadiri wanavyopata muda wa kucheza wanazidi kuimarika.

Akizungumzia ushindi wa mabao 2-0 tuliopata dhidi ya Dodoma Jiji, Robertinho amewapongeza wachezaji kwa kuonyesha kiwango safi.

“Kwanza nawapongeza wachezaji kwa kucheza soka safi na kupata ushindi muhimu nyumbani. Kadiri siku zinavyozidi kwenda wachezaji wanazidi kuzoeana.

“Mimi ninatokea Brazil, nimecheza soka na sasa ni mwalimu mara zote naamini kwenye kucheza soka la kushambulia pamoja na kumiliki mchezo na hicho ndicho nataka wachezaji wangu wakifanye,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER