Robertinho: Tumeonyesha Ukubwa wa Simba

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema katika ushindi wa mabao 3-1 tuliopata dhidi ya Tanzania Prisons umeonyesha ukubwa na ubora wa timu yetu.

Robertinho amesema licha ya kufungwa bao la mapema wachezaji hawaku changanyikiwa badala yake walitulia na kucheza katika mipango ile ile tuliyokuwa tumepanga na huo ndio ukubwa.

Robertinho amewapongeza wachezaji kwa jinsi walivyocheza soka safi lililotupa ushindi mnono na alama tatu muhimu.

“Mchezo wa leo umeonyesha daraja la Simba lipo juu, tulifungwa bao la mapema lakini halikututoa mchezoni tulimiliki mpira kama kawaida tukasawazisha na kuongeza.

“Mara zote nasisitiza tunapaswa kucheza soka safi na kushinda na ndicho kilichotokea leo, nawapongeza wachezaji wangu kwa kazi kubwa waliyofanya,” amesema Robertinho.

Kuhusu mashabiki waliojitokeza kwa wingi Robertinho amesema “wamekuwa walitupa sapoti na mara zote wamekuwa upande wetu, tunawashukuru sana kwa hili.”

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER