Robertinho: Timu bora uwanjani imeshinda

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema tulikuwa bora zaidi ya Singida Fountain Gate na tumestahili kushinda ingawa ilikuwa kwa penati.

Robertinho amesema tulikuwa bora maeneo mengi tukitawala sehemu kubwa ya mchezo huku Singida wakicheza mpira wa kasi na kushambulia kwa kushtukiza.

Robertinho amewasifia wachezaji wetu kwa kazi kubwa waliyofanya huku akimvulia kofia mlinda mlango, Ally Salim kwa kufanikiwa kuokoa penati ya kwanza.

“Lazima nikubali tumepata upinzani mkubwa, Singida wamecheza vizuri lakini sisi tulikuwa bora zaidi yao. Naweza kusema timu bora imeshinda ndani ya uwanja,” amesema Robertinho.

Akizungumzia mchezo wa fainali dhidi ya Yanga siku ya Jumapili, Robertinho amesema utakuwa mgumu lakini tupo tayari kuwakabili.

“Itakuwa mechi ngumu, ni Derby na siku zote inakuwa hivyo. Tuna siku siku mbili za kujiandaa kabla ya mchezo,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER