Robertinho: Nimerudi na Hamasa kubwa

Kocha mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amerejea usiku wa kuamkia leo kutoka nchini Brazil akiwa na nguvu mpya pamoja na hamasa ya kazi.

Robertinho amesema kwa muda wote wa wiki moja aliyokuwa Brazil alikuwa akiwasiliana na wasaidizi wake na kushirikiana katika programu za mazoezi.

“Nafurahi nimerudi salama Dar es Salaam, nimerudi nikiwa na nguvu mpya pamoja na hamasa ya kazi.

“Nilikuwa nawasiliana na walimu waliopo pamoja na kusaidiana programu za mazoezi. Nilikuwa nafuatilia nikiwa huko, nafurahi kila kitu kimeenda sawa,” amesema Robertinho.

Robertinho pia amezungumzia mchezo wa Azam Sports Federation Cup dhidi ya Coastal Union uliopigwa Jumamosi iliyopita na kusema.

“Bila kujali timu imechezaje, kikubwa ni ushindi uliotuwezesha kufika hatua ya 16 hilo ndilo la msingi na Nimefurahi” amesema Robertinho.

Kuelekea mchezo wa Ijumaa wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Big Stars, Robertinho amesema “tunahitaji kushinda ili kuongeza morali kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya ambao unaofata.”

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER