Robertinho: Nimefurahi kuiwezesha timu kuingia makundi Afrika

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema lengo la kwanza lilikuwa kuhakikisha timu inaingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuitoa Power Dynamos na hilo limefanikiwa.

Robertinho amewapongeza wachezaji kwa kutokata tamaa hadi mwisho kwakuwa Power Dynamos ni timu bora na ilikuwa imejipanga vizuri.

Akizungumzia mchezo wenyewe Robertinho amesema ilibadili kumuingiza nahodha John Bocco kipindi cha pili kwakuwa aliwaona Dynamos wote wamerudi nyuma na waliziba mianya ya kupitisha pasi hivyo alitakiwa mtu wa kusimama na walinzi wao.

“Nimefurahi kwa hatua hii, nawapongeza wachezaji wangu kwa kazi kubwa waliofanya. Nawashukuru mashabiki, Waandishi wa Habari na kila mtu kwa kufika hatua hii.

“Baada ya wenzetu kupata bao walirudi nyuma wote ikawa ngumu kupitisha mipira ikabidi tumuingize Bocco kwakuwa ni mrefu na angeweza kucheza sambamba nao na tuliongeza kasi iliyosababisha kupatikana kwa bao la kusawazisha,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER