Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amechaguliwa kocha bora wa Ligi Kuu ya NBC wa mwezi Oktoba.
Robertinho amewapiku Miguel Gamondi wa Yanga na Abdulhamid Moalin wa KMC ambao ameingia nao kinyang’anyiro hicho.
Katika mwezi Oktoba Robertinho ametuwezesha kushinda mechi zote tatu tulicheza dhidi ya Tanzania Prisons (1-3), Singida Fountain Gate (1-2), na Ihefu (1-2).
Simba ndio timu pekee ambayo haijapoteza wala kutoka sare mchezo wowote na tumeshinda mechi zote sita tulizocheza.