Robertinho awapongeza wachezaji ushindi dhidi ya Wydad

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amewapongeza wachezaji kwa kufuata maelekezo waliyowapa katika ushindi wa bao moja tuliopata dhidi ya Wydad Casablanca kwenye mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Robertinho amesema tulicheza kwa mipango tuliyojiwekea tunaposhambulia na tukipoteza mpira.

Robertinho pia amewapongeza wapinzani wetu Wydad kwa kucheza vizuri kwenye kuzuia hasa wakijua wapo ugenini.

“Nawapongeza wachezaji wangu kwa kiwango safi, haikuwa mechi rahisi. Tumecheza na timu kubwa lakini tumefanya vizuri.

“Timu yetu inazidi kuimarika kila siku, tuna wachezaji bora, kwa sasa kila timu inayopangwa nasi inapaswa kutuheshimu kama ambavyo sisi tunawaheshimu,” amesema Robertinho.

Akizungumzia mchezo wa marudiano utakaopigwa wikiendi ijayo nchini Morocco, Robertinho amesema “kila mchezo una mipango yake na mbinu zake, tunarudi kwenye uwanja wa mazoezi kujiandaa na mchezo huo.”

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER