Robertinho awapongeza wachezaji kwa kuipigania timu

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amewapongeza wachezaji kwa kupambana hadi mwisho licha ya kutolewa na Al Ahly kwa faida ya bao la ugenini.

Robertinho amesema wachezaji wamepambana na walijitahidi kutafuta ushindi lakini mpira una matokeo ya kikatili wakati mwingine.

Robertinho amewapongeza pia Al Ahly kwa kufanikiwa kutinga nusu fainali ya African Football League (AFL) lakini wamepata upinzani stahiki kutoka kwetu.

“Tulifanya kila tulichopaswa kufanya kutafuta ushindi, wachezaji wamepambana hadi mwisho na tulicheza vizuri pia, haikuwa kazi rahisi, nawaongeza kwa hilo.

“Nawapongeza pia Al Ahly kwa kufanikiwa kutinga nusu fainali, huu ni mpira, tutajipanga wakati mwingine,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER