Robertinho awaamini wachezaji kuimaliza Azam Kesho

Licha ya kukiri utakuwa mchezo mgumu wa Derby ya Mzizima dhidi ya Azam FC kesho katika muendelezo wa Ligi Kuu ya NBC kocha mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema anawaamini wachezaji wetu watatupa furaha ya ushindi.

Robertinho amesema tumepata matokeo mazuri kwenye mechi za ligi zilizopita na tunajua umuhimu wake na tupo tayari kuhakikisha tunashinda.

Robertinho ameongeza kuwa amewasisitiza wachezaji mazoezini kuhakikisha tunatumia vizuri nafasi tunazo tengeneza na kuzuia pamoja tunaposhambuliwa.

“Tuna matokeo mazuri kwenye ligi, tunatakiwa kuongeza kupata matokeo bora, tumetoka kupoteza mechi mbili za Ligi ya Mabingwa hatutaki kupoteza tena kwakuwa itashusha morali yetu.

“Itakuwa mechi ngumu sababu ni Derby, Azam ni timu nzuri na tunaiheshimu lakini nawaamini wachezaji wangu watafanya vizuri,” amesema Robertinho.

Akizungumzia uwepo wa kiungo mkabaji, Sadio Kanoute ambaye alikosekana kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Raja Casablanca kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano, Robertinho amesema:

“Nimefurahi kwa Kanoute kurejea kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Azam kwakuwa ni mchezaji wa kikosi cha kwanza, uwepo wake unatupa machaguo mengi ya upangaji wa kikosi.”

“Pia Jonas Mkude ambaye alikuwa majeruhi nilimpa dakika 45 za mwisho kwenye mchezo uliopita na amefanya vizuri nimefurahi, anakuja kuongeza kitu kikosi,” amesema Robertinho.

 

 

 

 

 

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER