Rais Samia atupongeza kwa kuifunga Yanga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ametupongeza baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya watani wetu wa jadi Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Katika pongezi hizo alizotuma kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rais Samia amesema mchezo wa Derby unawakutanisha Watanzania wengi kwa wakati mmoja.

“Hongereni Simba kwa ushindi mliopata dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC. Upinzani wenu wa jadi uwanjani ni burudani inayowaleta pamoja mamilioni ya Watanzania kutoka katika kila kona ya nchi yetu, kwa namna ya kipekee,” ameandika Rais Samia.

Rais Samia ni mdau mkubwa wa michezo hata katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Kombe la Shirikisho amekuwa akitoa Sh. 5,000,000 kwa kila bao linalofungwa na wawakilishi wa Tanzania ili kuongeza hamasa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER