Queens yapata ushindi dhidi ya Ceasiaa

Timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens imefanikiwa kupata ushindi wa bao moja dhidi ya Ceasiaa Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliopigwa Uwanja wa Samora mkoani Iringa.

Katika mchezo huo uliokuwa mkali muda wote huku timu zote nikishambulia kwa zamu bao pekee lilifungwa na Aisha Mnuka dakika ya 10.

Mnuka alifunga bao hilo baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na winga Elizabeth Wambui.

Mshambuliaji Jentrix Shikangwa alishindwa kuendelea na mchezo na Nafasi Yake Kuchukuliwa na Joanitah Ainembabzi dakika ya 21 kufuatia kupata maumivu.

Kocha Mkuu Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Asha Djafari, Danai Bhobho, Elizabeth Wambui na Jentrix Shikangwa.

Na kuwaingiza Asha Rashid, Ritticia nabbosa, Mwanahamis Omary na Joanitah Ainembabazi.

Ushindi huu unatufanya kufikisha pointi 28 baada ya kucheza mechi 10 huku mzunguko wa pili ukiwa ndio umeanza.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER