Queens, Yanga Princess kupigwa kwa Mkapa Alhamisi

Mchezo dhidi ya watani wa wetu wa jadi Yanga Princess wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite Women’s Premier League (SLWPL) ambao awali ulikuwa haujapangiwa uwanja sasa utapigwa Alhamisi, Desemba 22 saa 11 jioni katika dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa watani wa jadi huwa unasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa soka nchini kwa kuwa unakutanisha timu zenye upinzani na ushindani katika kushindania ubingwa.

Mchezo huo utakuwa ni wa tatu kwa timu zote zikiwa na matokeo ya kufanana hatua inayoongeza hamasa ya mechi yenyewe.

Queens inaendelea na mazoezi katika viwanja vyetu vya Mo Simba Arena chini ya Kocha Mkuu Charles Lukula na wasaidizi wake kujiandaa na mchezo huo muhimu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER