Queens yaichakaza Yanga Princess

Kikosi chetu cha Simba Queens kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya watani wa jadi Yanga Princess katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) uliopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Aisha Juma alitupatia bao la kwanza dakika ya pili baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Esther Wambui kutoka upande wa kulia.

Aisha alitupatia bao la pili dakika ya 10 baada ya kupokea pasi kutoka Wambui kabla ya kutuliza na kupiga tiktak iliyomshinda mlinda mlango wa Princess.

Neema Paul aliipatia Princess bao la kwanza dakika ya 14 kwa kichwa kufuatia mlinda mlango wa Queens Carolyene Rufa kutoka golini bila kuchukua tahadhari wakati wa mpira wa adhabu unapigwa na Precious.

Vivian Corazone alitupatia bao la tatu dakika ya 49 kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi ya Elizabeth Wambui kwa mara nyingine.

Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa, Fatuma Issa, Aisha Juma, Ritticia Nabbosa, Asha Djafar na Danai Bhobo na kuwaingiza Diana Mnali, Koku Kipanga, Olaiya Barakat na Esther Mayala.

Ushindi huu unaifanya Queens kufikisha pointi tisa ikiwa kinara baada ya kushinda mechi zote tatu ilizocheza mpaka sasa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER