Queens Mabingwa Ligi ya Wanawake 2021/22

Timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens imetawazwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuifunga Mlandizi Queens mabao 2-1 katika Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.

Queens inayonolewa na kocha, Sebastian Nkoma imefikisha pointi 57 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ikiwa imebakiwa na mechi mbili.

Katika mchezo huo uliokuwa mgumu wenye upinzani mkubwa tulipata bao la kwanza kupitia kwa Asha Djafar kwa mkwaju wa penati dakika ya 31 kabla ya Mlandizi kusawazisha dakika ya 38 lililofungwa na Victoria.

Silvia Mwacha alitupatia bao la ushindi dakika ya 67 na kutuhakikisha ubingwa wetu wa tatu mfululizo wa michuano hii.

Kocha Nkoma alifanya mabadiliko mara moja tu ya kumtoa Amina Ramadhani na kumuingiza Olaiya Barakat.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER