Queens kuondoka kesho na matumaini kibao

Kocha Mkuu Charles Lukula amesema kikosi chake kitaondoka kesho alfajiri kuelekea nchini Morocco kikiwa na matumaini ya kufanya vizuri kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na maandalizi tuliyofanya.

Lukula amesema michuano itakuwa migumu na timu zote zilizofanikiwa kupata nafasi ya kushiriki zipo vizuri nasi tumejipanga kuhakikisha tunaenda kufanya vizuri.

Akizungumzia hali ya kikosi Lukula amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na nyota wote 25 ambao wamepangwa kusafiri wako kamili tayari kwa mashindano.

“Tunakwenda kwenye mashindano haya tukiwa tuko tayari, kikosi kipo kamili hakuna mchezaji yeyote ambaye ni majeruhi. Tumefanikiwa kupata mechi kadhaa za kirafiki kwa hiyo tuko tayari,” amesema Lukula.

Kwa upande wake Nahodha Opa Clement, amesema wachezaji wanajua malengo ni kuhakikisha tunafika nusu fainali ya michuano hiyo japo haitakuwa rahisi.

“Tunawashukuru viongozi wetu kwa sapoti kubwa wanayotupatia, wamekuwa wakiweka mazingira yetu ya kazi kuwa rahisi, kikubwa tunawaomba mashabiki waendelee kutuombea ingawa hawatakuwepo uwanjani,” amesema Opa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER