Queens Kibaruani tena Kesho Uhuru

 

Timu yetu ya Simba Queens kesho saa 10 jioni itashuka katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kuikabili Ceasiaa Queens kutoka Iringa kwenye mchezo wa Ligi ya Wanawake ya Serengeti Lite Women’s Premier League.

Queens itaingia kwenye mchezo wa kesho ikiwa kinara kwenye msimamo baada ya kufikisha pointi 19.

Queens itaingia katika mchezo wa kesho ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi mnono wa mabao 4-1 tuliopata dhidi ya Baobab Queens katika mechi iliyopita.

Maandalizi ya mchezo yanaendelea vizuri wachezaji wapo kwenye hali nzuri na baada ya kukaa kileleni kwa msimamo lengo ni kuhakikisha hatushuki hadi tutetee ubingwa wetu.

Ingawa Ceasiaa haipo juu au sio miongoni mwa timu zinazowania taji lakini tutaingia kwa kuiheshimu na kuhakikisha tunatumia vizuri nafasi tutakazopata.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER