Kikosi chetu cha Simba Queens leo kitashuka katika Uwanja wa Uhuru kuikabili The Tigers Queens katika mchezo wa Serengeti Lite Women’s Premier League (SWPL).
Tunaingia katika mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bao moja tuliopata katika mechi iliyopita dhidi ya JKT Queens.
Tunafahamu The Tigers hawapo kwenye nafasi nzuri katika msimamo lakini hatuwadharau tutaingia kwenye mchezo kwa kuwaheshimu ili kupata alama tatu.
Lengo letu ni kuhakikisha tunapambana kupata alama tatu katika kila mchezo ili kutetea ubingwa wetu ambao tunaushirikiria.
Tunaendelea kukaa kileleni mwa msimamo tukiwa na alama 23 baada ya kucheza mechi 10.