Queens kibaruani dhidi ya JKT Fainali Ngao ya Jamii

Kikosi chetu cha Simba Queens leo saa 12 jioni kitashuka katika Uwanja wa Azam Complex kuikabili JKT Queens katika mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii.

Michuano ya Ngao ya Jamii ndio mara ya kwanza kufanyika kwa upande wa timu za Wanawake na tunataka kuwa wakwanza kuchukua taji hilo.

Kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo na jana jioni kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mbweni Veterani kujiandaa na mtanange wa leo.

Nyota wetu wawili Asha Djafar na Joelle Bukuru ambao walikuwa na majukumu ya timu za taifa nao wamejiunga na timu tayari kwa mchezo wa leo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER