Preview: Simba vs Raja Casablanca

Kikosi chetu leo saa moja usiku kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Raja Casablanca katika mchezo wetu wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Tunaingia katika mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza ugenini dhidi ya Horoya uliopigwa wiki iliyopita kwa bao moja.

Mchezo wa leo ni wa kwanza wa nyumbani ambao tutacheza mbele ya mashabiki 60,000 ambao watakuwepo uwanjani kutupa sapoti.

Ushindi katika mchezo wa leo utatuweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa Kundi letu hasa kutokana na ubora wa wapinzani tunaokutana nao.

Hali ya Kikosi

Wachezaji wapo kwenye hali nzuri, morali ipo juu na wanafahamu ugumu na umuhimu wa mchezo wa leo na wapo tayari kupambana hadi jasho la mwisho kuwapa Wanasimba furaha.

Saido arejea kunogesha

Kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza amerejea kikosini baada ya kupona majeraha na yupo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo.

Saido alipata maumivu katika mchezo wetu wa ligi dhidi ya Singida Big Stars na aliikosa mechi ya kwanza ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya wiki iliyopita.

Ahadi ya Rais Samia yaongeza morali kwa wachezaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan juzi ametoa ahadi ya kutoa Sh. 5,000,000 kwa kila bao tutakalofunga kwenye mchezo wa leo.

Nahodha wa timu, John Bocco amesema kauli hiyo imewapa wachezaji morali kubwa na kujiona wana deni kubwa sio kwa Wanasimba bali kwa Watanzania wote.

“Ni kitu cha kipekee kwetu wachezaji kupokea kauli ya Rais wa nchi, ameonyesha anatujali na tumeichukua kama morali na tunamuahidi hatutamuangusha, hii sio kwa Simba tu bali ni Watanzania wote,” amesema Bocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER