Phiri, Kyombo kuongoza mashambulizi dhidi ya Eagle leo

Kocha Juma Mgunda ameanza na washambuliaji wawili katika mchezo wetu wa hatua ya pili ya Azam Sports Federation Cup ASFC dhidi ya Eagle FC utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Mgunda amewaanzisha Moses Phiri na Habib Kyombo kuongoza mashambulizi huku Nahodha John Bocco akianzia benchi.

Wawili hao watapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Clatous Chama na Pape Sakho.

Kocha Mgunda pia amewaanzisha walinzi wa kati Kennedy Juma na Mohamed Ouattara wakichukua nafasi za Henock Inonga na Joash Onyango ambao wamekuwa wakianza mara nyingi.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Beno Kakolanya (30), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Victor Akpan (6), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), Habibu Kyombo (32), Moses Phiri (25), Pape Sakho (10).

Wachezaji wa Akiba

Ally Salim (1), Erasto Nyoni (18), Nassor Kapama (35), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Nelson Okwa (8), John Bocco (22), Kibu Denis (38), Augustine Okrah (27).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER