Phiri kuongoza mashambulizi dhidi ya Geita

 

Kocha Mkuu Zoran Maki amempanga Moses Phiri kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Geita Gold utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 12 jioni.

Katika mechi mbili zilizopita dhidi ya St. George (Simba Day) na Yanga (Ngao ya Jamii) kocha Zoran alimpanga Habib Kyombo kuongoza mashambulizi lakini leo ameona Phiri atafaa zaidi.

Phiri atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Clatous Chama, Pape Sakho na Peter Banda.

Mlinda mlango namba moja, Aishi Manula amerejea kwenye milingoti mitatu baada ya kukosa mechi mbili zilizopita kutokana na kuwa majeruhi.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Henock Inonga (29), Mohamed Ouattara (33), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (10), Sadio Kanoute (13), Moses Phiri (25), Clatous Chama (17), Peter Banda (11).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Joash Onyango (16), Mzamiru Yassin (19), Nelson Okwa (8), Augustine Okrah (27), Dejan Georgijevic (7), Habib Kyombo (32), Kibu Denis (38).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER