Pablo: Tuko tayari kwa Ruvu Shooting

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema kikosi kiko tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa kesho Ijumaa katika Uwanja wa CCM Kirumba saa 10 jioni.

Pablo amesema wachezaji wanajitahidi kuonyesha walicho nacho mazoezini na morali ipo juu kuhakikisha tunapata alama zote.

Pablo ameongeza kuwa Ruvu ni timu nzuri na inacheza kitimu na aliwatazama kupitia mkanda wa video katika mchezo dhidi ya Yanga na anaamini itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kushinda.

Pablo ameenda mbali na kusema licha ya kuwakosa baadhi ya nyota wetu kwa sababu mbalimbali lakini haitupi chakujitetea kwakua Simba ni timu kubwa na ina wachezaji wengi bora.

“Tuko tayari kwa mchezo wa kesho, wachezaji kamili morali ipo juu na tumejipanga kuhakikisha tunashinda. Ruvu ni timu nzuri inacheza kitimu tunaamini watatupa mechi ngumu,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER