Pablo awamwagia sifa wachezaji ushindi dhidi ya Biashara

Kocha Mkuu Pablo Franco, amewasifu wachezaji kwa jinsi walivyojituma katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Biashara United tulioibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Pablo amesema tangu turudi kutoka Morocco katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatujapata muda wa kupumzika wala kufanya mazoezi lakini wachezaji walijituma muda wote kuhakikisha tunashinda.

Pablo ameongeza kuwa tulijua mchezo ungekuwa mgumu lakini tumepata pointi tatu muhimu na mabao matatu ambazo tulikuwa tunazihitaji na hilo ndilo jambo kubwa.

“Kabla ya yote nichukue nafasi hii kuwapongeza wachezaji, tumecheza katika mazingira magumu hatukupata muda wa kupumzika wala kufanya mazoezi ya utimamu wa mwili lakini tumefanikiwa kupata pointi tatu.

“Ni pointi tatu muhimu kwetu kwa sababu zinapunguza tofauti iliyopo na wanaoongoza pamoja kuongeza hali ya kujiamini kuelekea mchezo wetu unaofuata,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER