Pablo abadili mfumo kikosi dhidi ya Orlando

Kocha Mkuu Pablo Franco, amebadili mfumo wa uchezaji katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates utakaoanza saa moja usiku kwa saa Tanzania.

Pablo amewapanga mabeki watatu wa kati badala ya wawili kama ilivyozoeleka. Mabeki hao ni Joash Onyango, Henock Inonga pamoja na Pascal Wawa.

Katika eneo la kiungo wa ulinzi amewapanga Jonas Mkude na Sadio Kanoute huku Shomari Kapombe aliyepangwa kama winga wa kulia atakuwa anaingia kati pia kuongeza idadi ya viungo.

Mshambuliaji Chris Mugalu ataongoza mashambulizi akipata msaada wa karibu kutoka Pape Ousmane Sakho.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Israel Patrick (5),
Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Pascal Wawa (6), Henock Inonga (29), Shomari Kapombe (12), Jonas Mkude (20), Chris Mugalu (7), Sadio Kanoute (13), Pape Sakho (17)

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Mzamiru Yassin (19), Peter Banda (11), Taddeo Lwanga (4), Rally Bwalya (8), Medie Kagere (14), Kibu Denis (38)

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER