Oppah, Mawete wafunguka baada ya kupiga ‘hat trick’

Washambuliaji wetu wa Timu ya Wanawake Simba Queens, Oppah Clement na Mawete Musolo wameweka wazi kuwa furaha yao ni kuhakikisha timu inapata ushindi vitu vingine ni ziada.

Wawili hao kila mmoja amefunga mabao matatu ‘hat trick’ katika mchezo wa mwisho wa kundi A katika michuano ya Caf Women’s Champions League Cecafa Qualifier 2021 dhidi ya FAD FC ambao umemalizika kwa ushindi mnono wa mabao 10-0.

Kwa upande wake Oppah amesema haangalii sana yeye kufunga bali anafurahi anapoisaidia timu kupata matokeo ya ushindi.

“Nimefurahi kufunga hat trick lakini furaha yangu zaidi ni kuisaidia timu kufanya vizuri kwenye mashindano sababu lengo letu ni kuchukua ubingwa, hayo mengine ni ziada,” amesema Oppah.

Nae Mawete amesema ushindi mnono tuliopata umeongeza hamasa kwa wachezaji kuelekea mchezo wa nusu fainali kwani tumebakisha hatua chache kabla ya kuingia fainali.

“Kwa mshambuliaji kufunga hat trick ni jambo zuri na linafurahisha lakini cha kwanza ni ushindi wa timu. Ushindi wa leo umeongeza hamasa kuelekea mchezo wa nusu fainali,” amesema Mawete.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER