Onyango, Mzamiru, Okrah wachuana Tuzo Mchezaji Bora Oktoba

Nyota wetu watatu wameingia fainali ya kinyang’anyiro cha kutafuta mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month.

Wachezaji hao ni mlinzi wa kati Joash Onyango, kiungo mkabaji Mzamiru Yassin na kiungo mshambuaji Augustine Okrah.

Kabla ya kuchujwa na kubaki watatu walikuwa watano wakiwemo kiungo mshambuaji, Clatous Chama na mshambuliaji Moses Phiri.

Takwimu zao za mwezi Oktoba

Mechi Dakika Assist Mabao

Joash 6 540 0 0

Mzamiru 5 450 1 1

Okrah 5 366 2 2

Zoezi la kupiga kura limeanza tayari kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz na litakamilika Novemba 2 saa sita usiku kisha mshindi wa jumla atatangazwa.

Mshindi wa jumla atakabidhiwa fedha taslimu Sh milioni mbili na tuzo kutoka kwa wadhamini Wakuu Emirate Aluminium Profile.

SHARE :
Facebook
Twitter

5 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER