Ntibazonkiza Kiungo Bora NBCPL

Kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza amechaguliwa kiungo bora wa Ligi Kuu ya NBC 2022/23 katika hafla ya tuzo za TFF zinazoendelea jijini Tanga.

Ntibazonkiza amewapiku nyota wengine Clatous Chama, Mzamiru Yasin Aziz Ki (Yanga) na Bruno Gomes (Singida Big Stars).

Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Ntibazonkiza ameitoa kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah ‘Try Again’ kwa kumuamini na kumsajili licha ya kusikia mambo mengi mabaya kumuhusu yeye.

“Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunifikisha hapa Uongozi wa Simba pamoja na Mwenyekiti Try Again kwa kuniamini mpaka kufika, hii tuzo ni kwa ajili yako,” amesema Ntibazonkiza.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER