Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho leo jioni katika Uwanja wa Boko Veterans kabla ya kuivaa TP Mazembe kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa Tamasha la Simba Day utakaopigwa kesho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Timu imefanya mazoezi kwenye uwanja huo kutokana na viwanja vyetu vya Mo Simba Arena kuwa katika matengenezo.
Advertisement
Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo mkubwa na kila mmoja amejaribu kumshawishi mwalimu ili ampe nafasi.
Kesho kwenye tamasha la Simba Day mashabiki na wapenzi watashuhudia kikosi kizima ambacho tutakitumika kwenye mashindano yote msimu wa 2021/22.