Mchezo wa utangulizi wa kirafiki kati ya timu yetu ya Wanawake Simba Queens dhidi ya Fountain Gate Academy umemalizika kwa sare ya bila kufungana.
Mchezo huo ulikuwa mzuri na wa kuvutia kutokana timu zote kucheza soka la kushambulia na kuwafanya mashabiki wengi waliojitokeza uwanjani kufurahi.
Advertisement
Hata hivyo safu yetu ya ushambuliaji iliyokuwa inaongozwa na Oppah Clement ilipoteza nafasi kadhaa za kufunga ambazo zingetufanya kuibuka na ushindi.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo sasa kinachoendelea hapa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ni burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva.