Baada ya kuwasili jijini Arusha kikosi chetu kitakuwa kinafanya mazoezi asubuhi na jioni kwa mujibu wa programu ya benchi la ufundi.
Kikosi kimewasili jana na leo kimefanya mazoezi ya asubuhi na jioni kikubwa ni kuendelea kutafuta stamina pamoja mbinu za uwanjani kwa muda wote tutakaokuwepo Arusha.
Meneja wa Timu Patrick Rweyemamu, amesema wachezaji wote 21 waliosafiri wapo kwenye hali nzuri na wale wageni wamezoeana na wenzao pamoja na mazingira ya timu.
"Kikosi kimewasili hapa Arusha jana usiku na kimeanza mazoezi asubuhi na jioni. Hatua hii ni kwa mujibu wa programu za mwalimu," amesema Rweyemamu.
Kikosi kinatarajia kucheza mechi kadhaa za kirafiki jijini Arusha kwa kadri ya maelekezo ya benchi la ufundi pamoja na upatikanaji wa timu husika.