Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Aga Khan jijini Arusha yakiwa ni mazoezi ya nwisho kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam tayari kwa Tamasha kubwa la kihistoria la Simba Day litakalofanyika Septemba 19.
Kikosi kimekaa jijini humo kwa muda wa wiki mbili ambapo kimefanikiwa kupata mechi tatu za kirafiki za kuwafanya wachezaji waendelee kuzoeana.
Advertisement
Kambi ya Arusha ni ya pili kwa timu yetu baada ya ile ya kwanza ya siku 18 nchini Morocco ambapo nako tulipata mechi mbili za kirafiki.
Katika kilele cha Simba Day Jumapili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya sherehe za utambulisho wa wachezaji kikosi kitashuka dimbani kuikabili TP Mazembe kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa