Kikosi chetu cha Timu ya Wanawake cha Simba Queens kesho kitashuka kwenye Uwanja wa Kasarani kucheza na Lady Doves katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu wa Michuano ya Caf Champions League Cecafa Qualifier 2021 kivingine.
Katika mchezo huo ambao utapigwa saa saba mchana benchi la ufundi limepanga baadhi ya wachezaji ambao hawajapata nafasi kubwa ya kucheza michuano hii.
Lengo letu lililobaki ni moja kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho na kuchukua nafasi ya tatu ingawa haitakuwa kazi rahisi.
Katika mchezo wa kesho tutamkosa nahodha wetu Violeth Nicholaus ambaye ni majeruhi baada ya kuumia katika mechi iliyopita dhidi ya Vihiga Queens.
Mchezo dhidi ya Lady Doves utakuwa ni wa pili kukutana nao baada ya ule wa hatua ya makundi ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.