Simba Sports Club
Caf Women's

Kiungo Simba Queens aingia kikosi bora cha CECAFA

14 Sep 2021

Kiungo wa timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens, Danai Bhobho amejumuishwa kwenye kikosi bora cha michuano ya Caf Women's Champions League Cecafa Qualifier 2021 iliyomalizika wiki iliyopita nchini Kenya.

Danai ni mchezaji ambaye tumemsajili msimu huu kutoka nchini Zimbabwe kwa ajili ya michuano mbalimbali ikiwemo ligi ya Wanawake 'Serengeti Lite Women's Primier League'.

Advertisement

Kiungo huyo fundi ndiye mchezaji wetu pekee ambaye ameingia kwenye kikosi bora cha mashindano kutokana na ubora aliouonyesha licha ya ugeni wake kikosini.

Katika mashindano hayo yakiyofanyika kwenye viwanja viwili vya Nyayo na Kasarani jijini Nairobi hivi karibuni, kikosi chetu kimemaliza kikiwa nafasi ya nne.

Back to homepage
Share this story